Timbwili la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa mwandishi na kusema:
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na
ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja
jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Kufuatia taarifa hiyo, mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani
ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu
huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!
Mwandishi bila kuzubaa alianza kuchukua picha za tukio hatua kwa hatua. Wakati Timbwili
likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo
amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo
zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.
Katika hali ya kushangza,
wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata
upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa
kamera.
Timbwili la wajomba hao
lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana) ambaye
alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.
Baada ya
kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu
alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi
kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa
makusudi.
Baadhi ya waungwana
waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake
na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa
familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe.
Kufuatia maombi
ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba
wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin
fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea
mke wake.
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na
mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo
kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.
Hata hivyo,
taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph
alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa
wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.
No comments:
Post a Comment