
Mahakama
ya usuluhishi ya Michezo CAS imekubari kusikiliza rufani ya
mshambuliaji wa Zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa amesajiliwa na
Barcelona na Italoea maamuzi katika wiki ya pili ya Mwezi wa Nane .
Kwa
mujibu wa Adhabu iliyotolewa na Shirikisho la kimataifa la soka Fifa
katika kamati yake ya Nidhamu , Suárez amefungiwa kucheza mechi za
kimataifa kwa mechi tisa na kutoruhusiwa kujishughurisha na maswala
yoyote yanayohusiana na mpira wa Miguu ikiwemo kwenda kutazama mpira
kiwanjani kwa muda wa Miezi minne".
Katika
maamuzi yaliyotolewa na Fifa kuhusu Suarez , FIFA ilimkuta na hatia
Mshambuliaji huyo kwa kuvunja Kifungu 48,
Para ya Kwanza 1, sehemu ya Nne d katika sheria za nidhamu za Fifa (FDC)
(Uzalilishaji),na kifungu cha 57 (Kinachosimia tabia zisizokubarika
uwanjani kwa mchezaji mwenza ).
No comments:
Post a Comment