Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro George Kavishe (kushoto) na katibu wa Yanga Lawrance
Mwalusako (kulia) wakiwa wameshika vifaa ambavyo Yanga imekabidhiwa leo
kwa ajili ya msimu wa ligi 2013/14
Ikiwa
ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi
vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC
kwa ajili ya msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi
ujao.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema
“Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa
kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2013/14 ambayo bila shaka
itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa
siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri.
Ni matumaini yetu kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na
Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi
kongwe.”
Kavishe aliongeza kuwa Vifaa ambavyo wametoa ni pamoja na mipira,
viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na
vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga
kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.
Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na
kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani
kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika
kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza wajibu
wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha
tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.
Kavishe alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa
Simba na Yanga umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na
kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji
wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.
Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo
vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea
kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano
wetu na klabu hizi mbili maarufu.
“Tunawaomba mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono
bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada
kuwapa burudani na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha
mafanikio.”
|
No comments:
Post a Comment