Monday, 11 August 2014

KIONGERA AULA SIMBA, ALAMBA MKATABA WA MIAKA MIWILI

KIONGERA ALIPOWASILI JIJINI DAR.

Simba leo imefanikiwa kumnasa mshambuliaji Paul Modo Kiongera aliyekuwa akikipiga KCB ya Kenya.

Kiongera amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba akiwapiku washambuliaji wengine kutoka Botswana na Gambia waliokuwa wakiwania nafasi.
Raia huyo wa Kenya alionyesha uwezo mkubwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco ambayo Simba ililala kwa mabao 3-0, juzi Jumamosi.
Hivyo Kiongera amewapiku wengine wawili, Ousimane Manneh wa Gambia na Jerome Rama ambao waliitaka nafasi hiyo moja ya mchezaji wa kimataifa iliyokuwa imebaki.

No comments:

Post a Comment