Monday, 11 August 2014

KUTOKA ARSENAL HADI BARCELONA, WENGER ANAUZA TU

BARCELONA IMEONYESHA KUVUTIWA NA KAZI YA KOCHA ARSENE WENGER WA ARSENAL.ANGALIA NAMNA AMBAVYO IMEKUWA IKIBEBA WACHEZAJI WA CHAGUO LAKE.

KIONGERA AULA SIMBA, ALAMBA MKATABA WA MIAKA MIWILI

KIONGERA ALIPOWASILI JIJINI DAR.

Simba leo imefanikiwa kumnasa mshambuliaji Paul Modo Kiongera aliyekuwa akikipiga KCB ya Kenya.

Kiongera amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba akiwapiku washambuliaji wengine kutoka Botswana na Gambia waliokuwa wakiwania nafasi.
Raia huyo wa Kenya alionyesha uwezo mkubwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco ambayo Simba ililala kwa mabao 3-0, juzi Jumamosi.
Hivyo Kiongera amewapiku wengine wawili, Ousimane Manneh wa Gambia na Jerome Rama ambao waliitaka nafasi hiyo moja ya mchezaji wa kimataifa iliyokuwa imebaki.

Wednesday, 6 August 2014

Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.


Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.
Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.
Webb ambaye amepuliza kipenga kwa muda wa miaka 25 amestaafu baada ya kuchaguliwa kuwa afisa wa shirikisho la marefarii (Professional Game Match Officials Limited PGMOL).
Kabla ya kustaafu Webb alikuwa muamuzi katika mechi 500 za ligi ya Premia ya Uingereza mbali na zile za kuwania ubingwa wa FA.
Hata hivyo kilele cha tajriba yake ilikuwa fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 iliyoandaliwa huko Afrika Kusini .
Refarii huyo mwenye umri wa miaka 43 alianza kazi hiyo mwaka wa 1989.
"najivunia tajriba niliyonayo na sasa nawashukuru wenzangu kwa kunichagua kuwahudumia katika kazi hii mpya ," alisema Webb.
Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.
Webb amewahi kuamua fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya fainali ya ligi kuu ya premia ya Uingereza.
Katika kombe la dunia lililokamilika majuzi huko Brazil, Webb alimua mechi ya kundi Cha baina ya Colombia na Ivory Coast,na ile ya mchujo baina ya Brazil na Chile.
Amewahi tuzwa na malkia wa Uingereza mwaka wa 2011na tuzo la MBE .

Friday, 1 August 2014

Kenya yakata rufaa ya marufuku ya CAF


  
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya mwaka mmoja iliyopewa kocha wa timu ya taifa Adel Amrouche na shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Amrouche alipigwa marufuku hiyo baada ya kudaiwa kumtemea mateafisa msimamizi wa mechi baina ya Harambee Stars ya Kenya naComoros mwezi Mei.
katibu wa Shirikisho la soka la Kenya FKF Michael Esakwa ameiambia BBC kuwa tayari wameshatuma ombi la kukata rufaa kwa shirikisho la CAF .
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
"baada ya kuona video ya tukio hilo linalodaiwa kutokea baada ya mechi nina hakika kuwa hakuna aliyetemewa mate ''.
Sadfa ni kuwa kocha mkuu wa Comoros Amir Abdou amepuzilia mbali uwezekano wa tukio hilo akisema haiwezekani kuwa Amrouche alimtemea mate afisa huyo.
''Mimi mwenyewe nili kuwepo na pia nilitazama video na kwa hakika ninaunga mkono FKF maanake hii ilikuwa ni mechi ambayo tulishiriki.''
Ujumbe huo wa kocha Abdou ulimpiga jeki Esakwa ambaye anasema kuwa taarifa hiyo itakuwa kati ya habari watakazopendekeza kutumiwa katika rufaa hiyo.
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
Kufuatia marufuku hiyo ya Amrouche, Kenyasasa inamtegemea Kocha mbadala James Nandwa kuiongoza Kenya katika mechi ya mkondo wa pili ya kufuzu kwa mechi ya kuwania kufuzu kwa dimba la mabingwa wa Afrika dhidi ya Lesotho.
Mechi hiyo itachezwa wikiendi hii mjini Nairobi.
Kenya ilishindwa katika mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa nunge ugenini.

Tineja Mnigeria kupokonywa dhahabu


  
Tineja Mnigeria kupokonywa dhahabu leo
Tineja kutoka Nigeria mshindi wa nishani ya dhahabu ya unyanyuaji uzani Chika Amalaha, anatarajiwa kupokonywa medali yake ya dhahabu na kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote leo.
Hii ni baada ya chembechembe za dawa zilizopigwa marufuku kupatikana katika vipimo vya pili vya damu yake hii leo.
Tineja huyo mwenye umri wa miaka 16 aliwatamausha wapinzani wake aliponyanyua kilo 196 na kunyakua nishani ya dhahabu ya kitengo cha wanawake wasiozidi kilo 53.
Shirikisho la michezo ya madola linakutana hii leo kutoa tangazo hilo.
Mnigeria huyo alikuwa amesimamishwa kwa muda kushiriki mashindano yeyote hadi vipimo vya pili vifanyiwe uchunguzi.
Bara la Afrika lilipigwa na butwaa wachunguzi walipotangaza kuwa damu yake ilipatikana na chembechembe za dawa za kuongeza nguvu mwilini zilizopigwa marufuku za amiloride na hydrochlorothiazide.
Chika anatarajiwa kupokonywa dhahabu leo
Mkurugenzi wa mashindano hayo Mike Hooper likuwa mwanariadha wa kwanza kupatikana na doa japo kutokea wakati huo wanariadha wengine wamepatikana kutumia madawa hayo.
Mwanaridha wa mbio za mita 400 kutoka Wales Rhys Williams mwengine wa mbio za mita 800m Gareth Warburton pia wamepatikana walitumia madawa hayo yaliyopigwa marufuku.
Mwanariadha huyo chipukizi wa Nigeria alishinda medali ya dhahabu Ijumaa iliyopita huku Dika Toua akiipatia Papua New Guinea medali yao ya kwanza ye fedha kwenye michezo hii ya Jumuiya ya madola mwaka huu.
Santoshi Matsa wa India aliipatia medali ya Shaba.
Lakini sasa kudhibitishwa kwa makosa hayo ya Amalaha inamaanisha kuwa sasa Papua New Guinea ndio mshindi wa dhahabu huku India ikijinyakulia nishani yake ya fedha.
Wanariadha wote hao wanakanusha kutumia dawa yoyote iliyopigwa marufuku huku wakiwa wanafahamu
Shirikisho la kupambana na madawa ya kututumua misuli limekuwa likijaribu kukomesha utumizi wa madawa hayo kwa kuwapiga marufuku wanariadha waliopatikana na hatia kwa kipindi cha miaka miwili.