Jumatano, Septemba 3, 2014
Leo ni Jumatano tarehe 7 Dhilqaada 1435 Hijria, inayosadifiana na Septemba 3, 2014.
Siku kama ya leo miaka 96
iliyopita, Damascus mji mkongwe na wa kihistoria wa Kiislamu ulikaliwa
kwa mabavu na vikosi vya majeshi ya Uingereza. Moja kati ya malengo
makuu ya serikali za Ulaya Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ilikuwa
kuusambaratisha utawala wa Othmania, lengo ambalo baadaye lilifanikiwa.
Wakati utawala wa Othmania ulipokuwa ukisambaratika, maeneo yaliyokuwa
chini ya utawala huo moja baada ya jingine yalidhibitiwa na Ufaransa na
Uingereza, ambapo mji wa Damascus katika Syria ya leo, pia ulishambuliwa
na katika siku kama ya leo ukakaliwa kwa mabavu.
katika siku kama ya leo miaka
71 iliyopita, mkataba wa kusalimu amri Italia katika Vita Vikuu vya Pili
vya Dunia ulitiwa saini baina ya wawakilishi wa Italia na nchi
waitifaki. Kwa mujibu wa mkataba huo, Waziri Mkuu wa Italia alikubali
bila masharti kusalimu amri nchi yake na kwa utaratibu huo, mmoja wa
waitifaki muhimu wa Ujerumani ya Kinazi katika vita hivyo, akawa
ameondoka katika medani ya vita.
Na miaka 43 iliyopita, yaani
tarehe 3 Septemba mwaka 1971, nchi ya Qatar ilipata uhuru toka kwa
mkoloni Mwingereza. Katika karne ya 19, Qatar ilikuwa ikihesabiwa kuwa
sehemu ya Peninsula ya Kiarabu. Baadaye nchi hiyo ikatawaliwa na
kudhibitiwa na Ufalme wa Othmania. Hata hivyo kufuatia kudhoofika
utawala huo, Qatar ambayo kuanzia mwaka 1882 na kuendelea kivitendo
ilikuwa ikiendeshwa na Uingereza, mwaka 1916 nchi hiyo ya Kiarabu ikawa
imetambuliwa rasmi kuwa koloni la Muingereza. Hadi mwaka 1971 Qatar
ilikuwa bado inakoloniwa na Uingereza ambapo mwaka huo huo, kwa
ushirikiano wa viongozi wa eneo la pambizoni mwa kusini mwa Ghuba ya
Uajemi, likaundwa Shirikisho la Umoja wa Falme za Kiarabu. Hata hivyo
mnamo Septemba mwaka huo huo, yaani 1971, Qatar ilijiondoa katika
Shirikisho la Umoja wa Falme za Kiarabu na kujitangazia uhuru.
No comments:
Post a Comment