Wednesday, 17 September 2014
TEVEZ BADO MOTO, APIGA ZOTE MBILI JUVE IKIUA 2-0 ULAYA
MABAO mawili ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Muargentina Carlos Tevez usiku huu yameipa ushindi wa 2-0 Juventus ya Italia katika mchezo wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tevez aliyewahi pia kuchezea Manchester City, alifunga bao moja kila kipindi dhidi ya Malmo FF ya Sweden katika dakika za 59 na 90 na kukipa mwanzo mzuri Kibibi Kizee cha Turin katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu barani Ulaya.
Wana fainali wa michuano ya msimu uliopita, Atletico Madrid wamepata kipigo cha ugenini kutoka kwa Olympiacos ya Ugiriki cha mabao 3-2.
Mabao ya wenyeji yamefungwa na Arthur Masuaku dakika ya 13, Ibrahim Affelay dakika ya 31 na Mitroglou dakika ya 74 wakati ya wageni yamefungwa na Mario Mandzukic dakika ya 38 na Griezmann dakika ya 87.
Wana fainali wa michuano ya msimu uliopita, Atletico Madrid wamepata kipigo cha ugenini kutoka kwa Olympiacos ya Ugiriki cha mabao 3-2.
Mabao ya wenyeji yamefungwa na Arthur Masuaku dakika ya 13, Ibrahim Affelay dakika ya 31 na Mitroglou dakika ya 74 wakati ya wageni yamefungwa na Mario Mandzukic dakika ya 38 na Griezmann dakika ya 87.
![]() |
Carlos Tevez bado moto, amefunga zote mbili Juve ikiua 2-0 Ulaya |
DANNY WELBECK 'ALIVYOWAKERA' ARSENAL JANA...
MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Danny Welbeck jana alikuwa ana nafasi nzuri ya kuwa shujaa wa timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund, lakini akashindwa kuitumia.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka kwa wapinzani, Manchester United jana alienedelea kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha The Gunners na kocha Arsene Wenger akionyesha alimsajili kwa sababu alimuamini, lakini akashindwa kuwafurahisha mashabiki.
Muingereza huyo jana alipata nafasi tatu nzuri za kuifungia Arsenal mabao kuanzia mapema kipindi cha kwanza, lakini zote akashindwa kuzitumia, The Gunners wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund ugenini.
Dhahiri Welbeck anahitaji kujiuliza mno baada ya mechi ya jana, kwani iwapo atarudia makosa aliyoyafanya katika mchezo huo, atajitengenezea mazingira ya kuondoka kwenye kikosi cha kwanza Gunners.
Haamini macho yake; Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck akiwa amepiga magoti kwa masikitiko baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza jana
Dhahiri Welbeck anahitaji kujiuliza mno baada ya mechi ya jana, kwani iwapo atarudia makosa aliyoyafanya katika mchezo huo, atajitengenezea mazingira ya kuondoka kwenye kikosi cha kwanza Gunners.

Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck alipata nafasi nzuri ya kufunga hapa bao ambalo lingekuwa la kuongoza kwa Arsenal, lakini akakosa mpira ukimpita namna hii

Nyingine hii; Danny Welbeck akianguka chini na kumshuhudia kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller akienda upande mwingine wa lango na mpira ukitoka nje baada ya kushindwa kuunganishia nyavuni
Na hii tena; Welbeck akapata nafasi nyingine tena, lakini akapiga juu ya lango
WACHEZAJI MAN UNITED 'WAKESHA' KUANGALIA LIGI YA MABINGWA
KLABU ya Manchester United haimo kabia katika michuano ya Ulaya msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya saba katika Ligi Kuu ya England msimu uliopita.
Pamoja na hayo, wachezaji wake wameendelea kuonyesha mapenzi na michano hiyo baada ya kukubakli kuchelewa kulala, ili waangalie mechi za Ligi ya Mabingwa. Kipa David de Gea na baadhi ya wachezaji wenzake jana walipoteza muda kwa ajili ya mechi za Ulaya.
Kipa huyo wa kimataifa wa Hispania, ameposti picha akiwa na wachezaji wenzake Marcos Rojo, Rafael, Antonio Valencia, Andreas Pereira, Anderson, Angel di Maria, Ander Herrera na Juan Mata wakipata chakula huku wanaangalia mechi za Ligi ya Mabingwa.
Mzuia michomo huyo wa zamani wa Atletico Madrid ameposti picha hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter akiambatanisha na ujumbe: "Chakula cha usiku na timu"!.
Tuesday, 16 September 2014
Liverpool yarejea katika ligi kuu Ulaya

Baada ya miaka 5 nje Liverpool leo wanawakaribisha timu ya Lugorets Razgrad,ya Bulgaria Anflied.
Wednesday, 3 September 2014
Jumatano, Septemba 3, 2014
Leo ni Jumatano tarehe 7 Dhilqaada 1435 Hijria, inayosadifiana na Septemba 3, 2014.
Siku kama ya leo miaka 96
iliyopita, Damascus mji mkongwe na wa kihistoria wa Kiislamu ulikaliwa
kwa mabavu na vikosi vya majeshi ya Uingereza. Moja kati ya malengo
makuu ya serikali za Ulaya Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ilikuwa
kuusambaratisha utawala wa Othmania, lengo ambalo baadaye lilifanikiwa.
Wakati utawala wa Othmania ulipokuwa ukisambaratika, maeneo yaliyokuwa
chini ya utawala huo moja baada ya jingine yalidhibitiwa na Ufaransa na
Uingereza, ambapo mji wa Damascus katika Syria ya leo, pia ulishambuliwa
na katika siku kama ya leo ukakaliwa kwa mabavu.
katika siku kama ya leo miaka
71 iliyopita, mkataba wa kusalimu amri Italia katika Vita Vikuu vya Pili
vya Dunia ulitiwa saini baina ya wawakilishi wa Italia na nchi
waitifaki. Kwa mujibu wa mkataba huo, Waziri Mkuu wa Italia alikubali
bila masharti kusalimu amri nchi yake na kwa utaratibu huo, mmoja wa
waitifaki muhimu wa Ujerumani ya Kinazi katika vita hivyo, akawa
ameondoka katika medani ya vita.
Na miaka 43 iliyopita, yaani
tarehe 3 Septemba mwaka 1971, nchi ya Qatar ilipata uhuru toka kwa
mkoloni Mwingereza. Katika karne ya 19, Qatar ilikuwa ikihesabiwa kuwa
sehemu ya Peninsula ya Kiarabu. Baadaye nchi hiyo ikatawaliwa na
kudhibitiwa na Ufalme wa Othmania. Hata hivyo kufuatia kudhoofika
utawala huo, Qatar ambayo kuanzia mwaka 1882 na kuendelea kivitendo
ilikuwa ikiendeshwa na Uingereza, mwaka 1916 nchi hiyo ya Kiarabu ikawa
imetambuliwa rasmi kuwa koloni la Muingereza. Hadi mwaka 1971 Qatar
ilikuwa bado inakoloniwa na Uingereza ambapo mwaka huo huo, kwa
ushirikiano wa viongozi wa eneo la pambizoni mwa kusini mwa Ghuba ya
Uajemi, likaundwa Shirikisho la Umoja wa Falme za Kiarabu. Hata hivyo
mnamo Septemba mwaka huo huo, yaani 1971, Qatar ilijiondoa katika
Shirikisho la Umoja wa Falme za Kiarabu na kujitangazia uhuru.
Barcelona yaanza LALIGA kwa makeke, Messi ang’ara
Subscribe to:
Posts (Atom)